ACT Wazalendo yataka uchunguzi ofisi ya DED

11Jun 2023
Julieth Mkireri
MAGU
Nipashe Jumapili
ACT Wazalendo yataka uchunguzi ofisi ya DED

CHAMA cha ACT Wazalendo, kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Magu kufanya uchunguzi kuhusu uhamishaji wa Ofisi ya Mkurugenzi.

Zitto Kabwe.

Kimewataka wananchi kufahamu sehemu ilikohamishiwa na endapo ikibainika aliyelipwa fidia ni kiongozi wa umma, afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika Mjini Magu, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe, alisema wananchi pia, wanatakiwa kufahamu mchakato mzima hadi kuhamishwa kwa ofisi hiyo.

“Ni lazima watu wa Magu wafahamu nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na viongozi wa umma ni lazima wajue kwamba, wana wajibu wa kuheshimu sheria zilizopo,”alisema Zitto.

Kiongozi huyo alisema kuwa Kamanda wa TAKUKURU Wilaya hiyo endapo hatachukua hatua zinazotakiwa, chama hicho kitamshtaki ngazi ya taifa ili  kuchukuliwa hatua na ikiwezekana aondolewe na aletwe mwingine kufanya kazi.

Katibu wa Jimbo hilo, Robert Kitula, alisema msimu wa pamba unapofika wakulima huelezwa kwamba bei zitakuwa juu lakini wakati wa kuuza huwa kinyume chake.