Watanzania 20 wakabiziwa zawadi na Airtel

06Feb 2024
Maulid Mmbaga
DAR ES SALAAM
Nipashe
Watanzania 20 wakabiziwa zawadi na Airtel

KAMPUNI ya Simu ya Airtel imetoa zawadi kwa zaidi ya wananchi 20 kwa nyakati tofauti walizoshinda kwenye kampeni ya (Upige Mwingi) inayoendeshwa na kampuni hiyo ambayo itakapofikia tamati wanatarajia kuwapeleka Watanzania kadhaa kuangalia fainali ya AFCON nchini Ivory Coast.

Akizungumza leo mkoani Dar es Salaam, wakati wa hafla ya ugawaji wa zawadi hizo zikiwamo mipira, simu na televisheni, Meneja Uhusiano wa Airtel Jennifer Mbuya, amesema lengo la droo hiyo pia ni pamoja na kuiwezesha jamii kupata vifaa vitakavyowasaidia katika kuendesha shughuli za kujiingizi kipato kama pikipiki, bajaji na simu.

Amesema kampeni hiyo ilianza mwezi Januari mwaka huu na itaendeshwa kwa siku 90 katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye fainali za AFCON, akisisitiza kuwa kila mmoja anaweza kushiriki huku akitoa wito kwa Watanzania kuepuka matapeli ambao watawapigia simu na namba tofauti na 100.

“Mwanzo tulisisitiza kwamba tutakuwa na washindi ambao tutaenda nao AFCON na sasa washiriki wamekuwa ni wengi na mwisho wa wiki hii tunatarajia kwenda Ivory Coast, natumai wengi wanaangalia michezo hii imekuwa na ushindani mkubwa sana, tunaona uwezo wa Afrika, endeleeni kutumia huduma zetu twende pamoja,” amesema Jennifer.

Edwini Kimaro, mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni miongoni mwa washiriki sita wa kampeni hiyo waliopatiwa zawadi, ameishukuru kampuni hiyo kwa kuendelea kujali Watanzania, jambo linalowasaidia