Hayo ameyabainisha wakati akisikiliza kero za wananchi wa Kata ya Buswelu ili kuwasogezea huduma katika maeneo yao, ambapo amesema kuwa malalamiko ya sukari yamekuwa mengi na wafanyabiashara wameshapewa bei elekezi ya kuuza bidhaa hiyo hivyo wananchi wanapaswa kutoa taarifa ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Sukari tulikuwa tunanunua kwa shilingi 1800 hadi 2000 kwa kilo lakini imepanda mpaka shilingi 4000 hadi 5000 na wengine wanauza kwa bei zao wanazozijua serikali haijakaa kimya ili kumlinda mlaji, mwananchi kupitia Wizara ya Kilimo, Waziri ameomba kibali cha kufungulia na kutoa vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kama dharura ili kuziba mwanya wa viwanda vya ndani," amesema Masala
Amesema wapo wanaendelea kuficha sukari ndani ili waendelee kuiuza kwa bei ya juu zaidi hivyo watakao enda ndivyo sivyo na maelekezo ya serikali watakamatwa na kufikishwa mahakamani na kushatikiwa kama muhujumu uchumi na leseni yake ya biashara itafutwa.
"Kwa kuliona hilo serikali imetoa bei elekezi ambayo imetofautiana kimkoa,kwa Mkoa wa Mwanza kilo ya sukari inapaswa kuwa 2650 mpaka 3000, nawaomba wananchi watakaouziwa sukari kuanzia elfu 4000 na kuendelea watoe taarifa ili hatua zichukuliwe kwa wafanyabiashara hao ikiwemo kupelekwa mahakamani"anaeleza Masala.
Robert Willam ni mkazi wa Buswelu "A" ameleza kuwa upatikanaji wa sukari ni tatizo kubwa kwa sasa katika eneo lake wananunua kwa 4500 jambo ilo linawalazimu wananchi wenye watu wengi kuachana na matumizi ya bidhaa hiyo.
"Unanunua sukari kwa gharama kubwa unaitumia kwa siku tatu imeisha kipato chenyewe cha kuungaunga nimeamua kuachana nayo hadi itakapokuwa sawa mwanzo sikuwa na elimu kuwa nikipandishiwa bei nitoe taarifa tutasimama na ili kwa kuwa wanatuumiza sana" ameeleza









