Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi Mkandarasi Henan Highway Engineering Group Ltd ya nchini China kuanza kazi ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 77.6 kwa kiwango cha lami itakayogharimu Sh. bilioni 88, amesema Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuhakikisha wanamsimamia kikamilifu mkandarasi huyo na kukamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa na ubora.
Naye Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi aliwataka watanzania kuwa wamoja hasa katika suala la kuinua uchumi wa nchi kazi ambayo Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeianza kwa kushirikisha sekta binafsi katika uwekezaji wa uchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amesema katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan mkoa huu umepewa Sh. bilioni 210 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya barabara.









