Wakizungumza na NIPASHE, Jijini hapa jana baadhi ya wajasiliamali wafugaji wa kuku, wakulima wa mahindi, mbogamboga pamoja na wauzaji wa pembejeo za kilimo walieleza kuwa miongoni mwa changamoto wanazopambana nazo ni ushuru.
Mariam Juma alieleza kuwa Serikali ni vyema ikaangalia uwezekano wa kupunguza ushuru wa uagiziaji pembejeo za kilimo nchini na kudhibiti bei ili kumuwezesha mkulima kumudu gharama na kulima kilimo cha kisasa.
Julius Mhando alisema wajasiriamali wengi wadogo wanashindwa
kuendeleza sekta hiyo kutokana na gharama za pembejeo kuwa kubwa ambazo alidai zinatokana na ushuru wanaolipa waingizaji hao.
“Serikali ni vema ikapunguza kodi kwa pembejeo za kilimo na madawa lengo likiwa ni kuifanya sekta hiyo kuwa kimbilio la watu wengi hasa wenye kipato cha chini kuweza kumudu gharama za uendeshaji’ alisema Zaina Ramadhani.
Walieleza kuwa watu wengi wamekuwa wakikimbia sekta ya kilimo na ufugaji kutokana na kushindwa gharama za pembejeo za kilimo na kwamba serikali inawajibu wa kuangalia suala hilo ili kuwakomboa wajasiliamali katika umasikini wa kipato.
Hata hivyo vijana ndiyo walioonekana kuguswa na kero hiyo ambao
walidai kuwa ushuru umewafanya wengi wao kutokuwa na dhamira ya kweli ya kujishughulisha na ufugaji na kilimo cha mbogamboga kutokana ukubwa wa gharama za kodi za Serikali.










