-pamoja na Taasisi ya Kuboresha Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania (AMDT).
Hayo yamebainishwa leo mkoani Mbeya na Meneja wa kampuni hiyo inayojihusisha na uzalishaji wa mbegu mbalimbali ikiwemo za alizetu na mahindi, huku ikielezwa kuwa mafanikio hayo yametokana na uwekezaji wa Sh. bilioni nne uliofanywa na AMDT katika mradi wa uhamasishaji wa matumizi ya mbegu bora.
Amesema pamoja na uzalishaji kuongezeka lakini bado mbegu zilizopo hazitoshelezi kutokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha uhitaji, ikiwa ni matokeo ya kampeni ya mradi huo ambayo imesaidia kuleta muamko mkubwa kwa wakulima.
“Wakulima wameona hizi mbegu za alizeti zilivyo bora kwahiyo wameongeza mahitaji msimu huu wanahitaji mbegu zaidi baada ya kuona uzalishaji wake ulivyo, juzi tulienda Mkoa wa Rukwa wakilima walikuwa na hamu ya kutaka kujua kuwa mbegu watazipata kweli,” amesema na kuongeza;
“Mradi umesaidia kwa kiasi kikubwa idadi ya wakulima imeongezeka, kutoka 300 ambao wananufaika moja kwa moja kwenye mradi, kuna wengine zaidi ya 1,000 watanufaika kupitia mbegu tunazoendelea kuzalisha,” amesema Omari.
Hata hivyo, amewashauri wakulima mbalimbali kutumia mbegu bora ya alizetu kwasababu zote za msimu zimetoka katika taasisi za tafiti za hapa nchini kama TARI Ilongo, na kwamba zinaendana na kiwango cha kimataifa, na zinauwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
“Mbegu za aina ya RECORD ambazo zinazalishwa na TARI pia hazina magonjwa yanayosababisha mavuno yashuke, ukubwa wa kichwa cha ufuta ndio unaongeza mavuno na kiuchumi itamsaidia kurudisha gharama na kupata fedha ya zaidi," amesema Omari.










