Jukwa hilo la Uziduaji limefanyikia leo Novemba 9, 2023 Jijini Dodoma, ambalo limekutanisha wadau mbalimbali wa Sekta hiyo kutoka Asasi za Kirai, Wawakilishi wa Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Makampuni ya Madini, Wachimbaji Wadogo, Wawakilishi kutoka Jamii husika, Wanataaluma na Waandishi wa vyombo vya habari na litahimishwa kesho.
Kapinga akizungumza wakati wa kufungua Jukwaa hilo la Uziduaji akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Amesema Serikali inathamini mchango mkubwa wa Asasi za Kiraia katika Masuala ambayo yanahusu Maendeleo ya Watanzania, na kupongeza Jukwaa hilo la Uziduaji ambalo litajadili mustakabali wa Maendeleo ya nchi.
Amesema Wizara ya Nishati vyanzo vyake vya kuzalisha Umeme vinahusiana na Sekta hiyo ya Uziduaji hususani kwenye gesi, na kubainisha kuwa Jukwaa hilo ni muhimu kwao kama Wizara.
“Mikutano ya namna hii inatusaidia Serikali kuweza kuboresha mipango yetu ili kuweza kuwanufaisha Watanzania kupitia Rasirimali za Nchi,”amesema Kapinga.
Aidha, amesema Serikali kupitia Nishati ya Umeme wameendelea kuboresha vyanzo vya Gesi, kwa kusafisha visima vya gesi vilivyopo Songosongo, Mnazibei, na Madiba, ilikuweza kuzalisha Gesi kwa kiasi kikubwa na kuzalisha Umeme ilikuondokana na changamoto ya Tatizo la Umeme hapa nchini.
Naye Mkurugenzi wa HakiRasilimali Adam Anthony, amesema Jukwaa hilo la Uziduaji yani Madini, Mafuta na Gesi Asilia, nila 13 ambalo wamekuwa wakijadili masuala mbalimbali katika Sekta hiyo, ili kuongeza Uwazi na Uwajibikaji kwa Maendeleo ya Sekta na Taifa kwa ujumla.
“Mwaka huu Jukwaa la Uziduaji tuna adhimisha chini ya Kaulimbiu isemayo” kufanikisha Mhamo wa Nishati na Mendeleo endelevu katika Sekta ya Uziduaji Tanzania,”amasema Anthony.
Aidha, amesema katika Siku hizo mbili watajadili kwa kina Ushiriki wa Wazawa katika Mnyororo wa thamani, ‘Local Content’, Mazingira Rafiki ya Uwekezaji, Haki za Binadamu, Uwazi wa Mikataba, Utoaji Lesseni, Ushiriki wa Wanawake katika Sekta na nafasi ya wachimbaji wadogo.










