SBL kuwawezesha vijana kushiri katika sekta ya kilimo

05Jun 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
SBL kuwawezesha vijana kushiri katika sekta ya kilimo

WANAFUNZI 27 kutoka katika Chuo cha Kilimo na Mfugo Kaole kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani wamekabidhiwa vyeti vya ufadhili wa masomo na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ili kuwawezesha vijana kuwa na ushiriki mpana zaidi katika kilimo.

Makamu mkuu wa chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani Maximillian Sarakikya (wa tatu kulia) akiwaeleza kitu baadhi ya wafanyakazi kampuni ya bia ya Serengeti waliotembelea chuo hicho mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha ni wanafunzi wa chuo hicho ambao ni wanufaika na programu ya ufadhili wa masomo inayojulikana kama Kilimo Viwanda.

Akiongea jana wakati wa kukabidhi vyeti hivyo katika chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole, chini ya programu ya Kilimo Viwanda,  Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL, John Wanyancha alisema, SBL inatambua umuhimu wa vijana kushiriki katika kilimo.“Vijana ambao tunawafadhili chini ya programu ya Kilimo viwanda, watakwenda kuongeza nguvu kwenye sekta hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu. Mchango wao utakuwa muhimu sana katika kuhakikisha kilimo chetu kinakuwa na tija,” alisema Wanyancha.Wanyancha alisema kuwa SBL hutumia malighafi zinazotokana na kilimo kutengenezea bia zake ikiwa ni pamoja na shayiri, mtama na mahindi na kuongeza kuwa uwepo wa wataalamu wa kutosha utasaidia upatikanaji wa malighafi hizo ambazo mahitaji yake yamekuwa yakiongezeka.

Mkuu wa idara ya kilimo wa chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani Fadhili kilikaya (Kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi ya wafanyakazi kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) waliotembelea chuo hicho mwishoni mwa wiki. Katika ziara hiyo wafanyakazi wa SBL waliwakabidhi vyeti wanafunzi 27 wa chuo hicho wanaopata udhamini wa masomo kupitia programu ya Kilimo Viwanda vya kampuni hiyo.

“Mahitaji yetu ya malighafi yanaongezeka kila mwaka. Mwaka 2021 kwa mfano tulinunua tani 18 za malighafi ambazo ni sawa na asilimai 80 ya mahitaji yetu kwa mwaka. Lengo letu ni kufikia asilimia 85 ifikapo mwaka 2025,” alielezaKupitia programu ya kilimo Viwanda, SBL tayari imeshatoa ufadhili kwa wanafuzi zaidi ya 200 wanasomea masomo ya kilimo katika vyuo vinne ambavyo ni Kaole cha Bagamoyo, Kilacha cha Moshi, Mt. Maria Goretti cha Iringa na Igabiro kilichopo Muleba mkoani Kagera.Mkuu wa chuo cha Kaole, Sinani Simba aliishukuru SBL kwa kutoa ufadhili kwa wanafunzi ambao amesema pasipo msaada huo wengi wao wangeshindwa kumaliza masomo yao kutokana na changamoto ya kushindwa kulipa ada.“Mchango wa SBL siyo tu unawasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia duni kupata fursa ya kuendelea na masomo, bali pia unasaidia kukuza sekta ya kilimo hapa nchini kupitia kuongeza wataalamu ambao takwimu zinaonyesha ni wachache ukilinganisaha na mahitaji,” alisema.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi na wanafunzi ambao ni wanufaika wa programu ya ufadhili wa masomo ya kilimo unaojulikana kama Kilimo Viwanda kutoka  Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole wazazi kilichopo Bagamoyo muda mfupi baada ya kuwanyakazi wa kampuni hiyo kutembelea chuo hicho.