Akizunguza katika maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya EFG, ambayo yamefanyika Dar es salaam (UDSM) jana Oktoba 31, 2023, alisema kuwa katila kipindi hiki ambacho teknolojia inakuwa ni mhimu kewnda sambamba nayo ili kuleta Maendeleo.
Pia aliwaasa Wanawake ambao ni wanufaika wa programu hiyo kuepukana na mikopo ambayo inawaletea changamoto na kuwarusisha nyuma.
"Mikopo maarufu kama kausha damu hii ni hatari kwenu chukueni mikopo inayowanufaisha na sio mikopo inayowadidimiza na kuwaletea migogoro kwenye jamii" alisema Hangi.
Aidha Program ya Mwanamke Sokoni imetengezwa katika mikoa tisa ya Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Mwanza, Shiyanga, Lindi, Mtwara, Mbeya, Iringa Tanga katika Wilaya ya Lushoto na Mkoa wa Mara huku lengo ikiwa ni kutoa fursa kwa mikoa yote ya Tanzania Bara.
Pia programu hii imemuwezesha Mwanamke kushika nafasi za uongozi sokoni na kongeza ujuzi na kusaidia Wanawake kujiamini katika kuongoza kwenye nafasi mbalimbali"
Naye Mwakilishi kutoka taasisi ya Digital Brain, Mbuto Chibwaya ametumia nafasi hiyo kuwasihi Wanawake juu ya umuhimu wa teknolojia katika kukuza biashara zao, ambapo amesema kuwa kutoendana na teknolojia kunaweza kuleta utofauti mkubwa baada ya miaka michache ijayo kwamba waliotumia vyema fursa ya teknolojia wanakuwa katika nafasi nzuri ya kuwaacha nyuma wale ambao wameshindwa kwendana nayo.
Taasisi ya EFG imekuwa ikishughulika na kuwainua Wanawake kiuchumi hususani walioko masokoni na kuchochea mabadiliko ya sheria ili kuwawezesha Wanawake kuendelea kuinuka kiuchumi na kukuza masuala ya kijinsia hususani Wanawake kuwa sehemu ya uongozi katika ngazi mbalimbali.










