Mshindi wa Sh. 500,000 wa maokoto ya Serengeti akabidhiwa zawadi yake

10Dec 2023
Na Mwandishi Wetu
Morogoro
Nipashe Jumapili
Mshindi wa Sh. 500,000 wa maokoto ya Serengeti akabidhiwa zawadi yake

Washindi mbalimbali wanaendelea kujishindia maokoto kupitia vizibo, zoezi linaloendeshwa na Kampuni ya Serengeti Breweries.

Mshindi wa shindano la Maokoto kutoka Wilaya Kilosa linaloendeshwa kupitia vizibo vya vinywaji vya kampuni ya bia ya Serengeti SBL, Martha Manywa (kulia) akipokea hundi ya mfano ya TSh 500,000 kutoka kwa Shomari Mohammed Mwakilishi wa mauzo wa kampuni ya SBL (kushoto), hafla ya kukabidhi zawadi hiyo imefanyika katika bar ya Comer Pub iliopo Dumila Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro siku ya ijumaa.