Katika uchaguzi huo Mhandisi Gabriel alibuka mshindi kwa kura (20) kati ya wapiga kura 24 huku mpinzani wake Gaudensia Damas akiibuka na kura 4.
Mwenyekiti huyo mpya amesema kuwa atashirikiana na serikali na kuhahikisha wafanyabiashara wa mkoa huo wanafikia dira mpya maendeleo ikiwemo kuhamasisha ujenzi wa viwanda na kuinua Uchumi wa mkoa huo .
Awali Katibu Mkuu wa chemba hiyo Mkoa wa Geita, Mariam Mkaka amesema uchaguzi huo umefanyika kufuatia aliyekuwa mwenyekiti wa chemba hiyo George Mandia kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ambapo aliongeza kuwa viongozi hao wa mpito wataingoza hadi mwezi machi mwaka 2024 utakapo fanyika uchaguzi mkuu wa chemba hiyo.
Katibu huyo amasema kuwa viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti Biashara Raphael Siyantemi, Makamu Mwenyekiti Viwanda Marth Komba, Makamu Mwenyekiti Wanawake Anifa Mfuruki na wajumbe wa chemba hiyo.










