KIBO GOLD yarudi tena Kanda ya Kaskazini 

28Jul 2023
Na Mwandishi Wetu
MOSHI
Nipashe
KIBO GOLD yarudi tena Kanda ya Kaskazini 

Wakazi wa kanda ya mikoa ya kaskazini ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro wamekoshwa baada ya bia ya KIBO GOLD kurudi tena baada ya kukosekana kwa kipindi cha miaka mitano sokoni. 

Viongozi wa SBL wakitoa ishara ya kutangaza rasmi kurejea kileleni kwa bia ya KIBO GOLD

Kurudi tena kwa bia hiyo inalenga kudumisha historia ya kipekee kwa SBL kutengeneza bia yenye kilele cha ladha ileile bora na adimu ambapo pia chapa hii imeshuhudiwa kunyakua tuzo mbalimbali za dhahabu kama ya Monde Section kwenye mashindano yaliyofanyika mjini Bordeaux, nchini Ufaransa mwaka 2014.

Bia ya KIBO GOLD sasa inarejea ikiwa na mwonekano maridadi kwa kutengenezwa kwa ubora usio na kifani – ikiwa na viungo vya asilia na kutokuwa na sukari ya ziada na kwa bei ya 1,500/- tu.

Akizungumza katika uzinduzi wa bia hio mwanzoni mwa wiki hii mjini Moshi, Meneja Uvumbuzi wa SBL, Bertha Vedastus, alisema,.. ‘’Kama SBL tunalenga kupanua wigo wetu wa bidhaa kuhakikisha tunakidhi mahitaji ya wateja wetu popote walipo.Na kama tunavyojua watanzania tunathamini sana urithi na utamaduni katika kila jambo tunalolifanya.

Hivyo basi, tunapotafuta maendeleo katika maisha yetu ya kila siku, ni muhimu kuhifadhi na kuthamini urithi na utamaduni wetu. Na kwayo, uwepo wetu wa muda mrefu katika kanda ya Kaskazini umetufanya kuja na maamuzi ya kina ya kudumisha urithi na ufahari wa kanda hii kupitia bia ya KIBO GOLD," alisema. 

Wafanyabiashara mbalimbali wakiburudika na bia hio wakati katika hafla hio iliyofanyika mjini Moshi.

Bertha aliendelea kuelezea kuwa bia ya KIBO GOLD ina utajiri wa kihistoria na urithi wa ubora ambao kila mtanzania inabidi ajivunie kuuendeleza. Alinukuliwa, "Ni bia yetu, ya watu wetu na urithi wetu. Tunaamini KIBO GOLD - Kilele Cha Ubora, itaendelea kuwa chaguo la kwanza kwa wapenda bia katika kanda hii nzima,’’.

SBL baada ya kutambua mara moja uwezo na thamani ya chapa hiyo ya KIBO GOLD imedhamiria kuirejesha katika mioyo ya wapendwa wa bia kote Ukanda wa Kaskazini. Bia hii yenye sura mpya ya kisasa kwa bia itaongeza mvuto wake kwa soko la ndani na la nje.

Meneja Uvumbuzi kutoka SBL, Bertha Vedastus (watatu kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika tukio la kutangaza kuirudisha tena bia ya KIBO GOLD kanda ya kaskazini. Wa kwanza kulia ni Meneja Chapa Uvumbuzi, Joseph Innocent, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uvumbuzi, Anitha Rwehumbiza. Wa kwanza kushoto ni Meneja Masoko kanda ya kaskazini, Andrew Msiagi, wa pili kushoto ni Meneja Mauzo kanda ya kaskazini, Patrick Kisaka na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara, Chris Gitau.