-inayofanywa na mafundi jamii, maarufu force account.
Dk. Timbuka, amewataka mafundi jamii hao, kuzingatia vigezo vya ubora na kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo kwa wakati, alipotembelea na kukagua shule tano za sekondari na saba za msingi.
Amesema hayo jana Julai 13, 2023 wakati alipotembelea Shule za Sekondari za Karansi na Namwai, ambapo amesema katika Mradi wa Uboreshaji Elimu ya Sekondari (SEQUIP), serikali imeitengea Wilaya hiyo, Sh.bilioni 2.32, wakati Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST), imetengewa Sh. milioni 999.
“Naagiza mafundi wote wanaojenga miradi ya miundombinu na vyumba vya madarasa, muongeze juhudi za ujenzi, lakini kwa kuzingatia ubora na muda uliopangwa, kwa ajili ya ukamilishaji ili ifikapo Agosti 13 mwaka huu wanafunzi wote walichaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika Wilaya yetu waweze kuanza masomo. Nimeambiwa kila shule inategemea kupokea wanafunzi wasiopungua 320"










