Amesema, aina hiyo ya bima ina umuhimu wa kipekee hasa tatizo linapojitokeza ikiwamo kupoteza maisha.
Akizungumza jana jijini hapa katika mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Madaktari Tanganyika (MAT), alisema bima ina umuhimu katika fani ya utabibu hususani wakati wa utafiti wa dawa.
"Kikubwa nawaomba watu tuwe na utamaduni wa kuweka bima za maisha hasa madaktari. Wengi wako kwenye uchunguzi wa dawa, hivyo kupata athari ni muda wowote na unapokuwa na bima utapata huduma sahihi," alisema.
Pia alisema, alisema katika mkutano huo, wanatangaza huduma mpya ya bima ya Beam Life ambayo imejikita kwenye uwekezaji.
Alisema, bima hiyo tofauti na zingine zaidi ya 25 walizo nazo, inasaidia mtu kutimiza ndoto zake za kujenga nyumba, kuanzisha kliniki au ununuzi wa vifaa vya afya pale atakapotimiza muda uliowekeza.
Polepole alisema, NIC limejipanga vyema kutoa huduma mbalimbali zinazoendana na jamii ikiwa ni kuongeza hamasa kwa jamii kuweka utaratibu wa kukata bima.
Aliyekuwa Rais wa MAT, Dk. Elisha Osati, alisema katika mkutano huo suala la bima ya afya limetiliwa mkazo na kuhimizana kujiunga na huduma hiyo.
"Maana tunaamini mgonjwa akiwa na bima tutamuhudumia ipasavyo na kwa undani, sababu hana kikwazo cha fedha," alisema.
Dk. Osati alisema, ni muhimu kwa kila mtu kujitafakari kwenye familia yake na kuchukua hatua za kuwa na bima hizo ili kuondokana na msongo wa mawazo pale inapotokea shida ya kiafya kwa mwanafamilia.
Pia, aliomba kila Mtanzania kuhakikisha anachukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ulioanza kuripotiwa wilaya ya Mubende nchini Uganda.
"Endapo ntu ataona dalili za ugonjwa huu anatakiwa kwenda kwenye vituo vya afya au hospitali haraka na ikiwezekana mtu ajitenge mwenyewe kulinda wengine na uzuri njia za kujikinga na ugonjwa huu ni kama zile za UVIKO-19," alisema.










