Benki ya NMB imeandika historia

18Jun 2023
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Benki ya NMB imeandika historia
  • Yamkabidhi Rais Samia gawio la Sh.bilioni 45.5

 
Benki ya NMB imetoa gawio la Sh.bilioni 45.5, ikiwa ni gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na taasisi ya kifedha kwa serikali.

Gawio hilo kwa serikali ni kiashiria tosha cha Azma ya benki hiyo ya kuhakikisha inaleta tija na faida kubwa kwa wawekezaji wote wa benki hiyo, ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo,Dk. Edwin Mhede pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu - Ruth Zaipuna, jana walimkabidhi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya gawio hilo katika sherehe ya maadhimisho ya mikaa 25 ya mafanikio ya Benki ya NMB, inayoendela katika ukumbi wa Mlimani City – Dar es Salaam. 

Katika picha walioshuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba pamoja na viongozi wengine wa serikali.