Bashe awataka radhi wakulima wa parachichi

07Aug 2022
Na Mwandishi Wetu
Mbeya
Nipashe Jumapili
Bashe awataka radhi wakulima wa parachichi

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, amewaomba radhi wakulima wa zao la parachichi wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa tatizo lililotokea msimu wa kilimo uliopita kuwa halitojirudia tena.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Bashe amesema hayo leo Agosti 7, 2022 alipopewa fursa na Rais Samia Suluhu Hassan kusalimia wananchi wa Kiwira wilayani humo katika ziara ya Mkuu huyo wa nchi mkoani Mbeya.

Bashe ameeleza msimamo wa Serikali kubadili mifumo ya ununuzi pembejeo za kilimo za ruzuku baada ya Serikali kuja na mpango wa ujenzi wa viwanda vya mbolea nchini.

"Niwaombe radhi wakulima wa parachichi Wilaya Rungwe kwani msimu uliopita wa kilimo hali ilikuwa mbaya na changamoto kubwa ikiwa ni gharama za pembejeo za kilimo kuwa juu," amesema Waziri Bashe.