Airtel yatoa Sh. bilioni tatu gawio la Airtel Money

10Feb 2016
DAR
Nipashe
Airtel yatoa Sh. bilioni tatu gawio la Airtel Money

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza kutoa gawio la faida kwa wateja wake wa Airtel money zaidi ya milioni sita, pamoja na mawakala wake nchi nzima.

Meneja wa kitengo cha Airtel money, Asupya Naligingwa.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza kutoa gawio la faida kwa wateja wake wa Airtel money zaidi ya milioni sita, pamoja na mawakala wake nchi nzima.

Airtel italipa gawio la faida iliyopatikana kwa watumiaji wa huduma ya Airtel money kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Desemba 2015, ambapo kila mteja wa Airtel money atapokea gawio lake kulingana na kiasi cha salio lake katika akaunti yake ya Airtel money kila siku.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, meneja wa kitengo cha Airtel money, Asupya Naligingwa, alisema: “Tunayofuraha kubwa kutangaza mpango wetu wa kugawa faida ya Shilingi 3,287,107,061 kwa watumiaji wa huduma yetu ya Airtel money pamoja na mawakala nchi nzima.”

“Hii ni mara ya pili kwa kampuni yetu kutoa gawio kwa wateja watu. Mwaka jana tulitoa kiasi cha jumla ya Shilingi bilion 5.3,” alisema.

Naligingwa aliongeza kuwa: “Tunaamini gawio hili la faida litawasaidia mamilioni ya wateja wetu kufanya mambo mbalimbali kulingana na mahitaji yao na hivyo kudhihirisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora za kifedha nchini.”

Huduma ya Airtel money inawawezesha wateja kulipia ankra za huduma na bidhaa, kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi vya data, kutuma na kupokea pesa, kutoa pesa kwenye akaunti zao za Airtel money na kutoa na kutuma pesa kutoka kwenye akaunti zao za benki.