Hoteli hiyo ijulikanayo kwa jina la Konokono iliyoko Michamvi, mkoa wa Kusini Unguja, inamilikiwa na watu watatu, akiwamo Amina Karume, kwa mara ya kwanza iliungua wiki iliyopita.
Akizungumza na Nipashe jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Juma Saadi Khamis, alisema chanzo cha moto huo hakijajulikana na kwamba uchunguzi unaendelea.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, tukio hilo limetokea juzi saa 4:30 asubuhi na kuunguza vyumba viwili.
Wakati ilipoungua awali, uvumi ulizagaa kwamba tukio hilo lina mkono wa kisiasa, lakini baadae jeshi la polisi lilikanusha baada ya kufanya uchunguzi na kusema lilisababishwa na cheche za moto zilizoruka kutoka jengo la jirani.










