Akiitambulisha kampeni hiyo, leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo, amesema lengo la kuja na kampeni hiyo ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
"Dunia ya sasa hivi imebadilika tunataka kuona jeshi la wanawake likiwa kidigitali...hii itasaidia kujua tuna wanawake wangapi na jinsi ya kuweza kuwasaidia," amesema Jokate.
"Tumetoa maagizo kwa makatibu wa kila mikoa kulisimamia hili kuhakikisha wanawake wote wanajisajili. Na tunatoa wito kwa wanawake nchi nzima kujitokeza kwa wingi kujisajili kidigitali," amesema Jokate.
Aidha, Jokate ametoa wito kwa UWT kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu, kutokana na jitihada anazozifanya za maendeleo nchini.
Hata hivyo, Jokate amehamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi hususani katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
"Katika uchaguzi tutahakikisha wanawake wanajitokeza katika nafasi mbalimbali. Lazima tukagombee kwenye nafasi hizo, kwani takwimu zilizopo hata asilimia 10 hatujafikia," amesema
"Ifike mwisho wanawake kuwa ndugu watazamaji, tunaye kinara wetu Rais Samia tutahakikisha kama kuna mwanamke anagombea anapitishwa na Chama na anashinda. Tutakesha kwenye Mitaa kuhamasisha wanawake kugombea na ninaomba niwatie moyo wanawake, hii ni fursa na akitokea mwanamke kugombea tusimkatishe tamaa tumpiganie apate ushindi," amesema Jokate.
wakati huo huo Jokate amezindua kundi la Samia Queen ambalo linauganisha wasanii na waigizaji wa kike nchini ambao wametunga nyimbo ya kuhamasisha wanawake kujikwamua kiuchumi.
Amesema katika kuelekea siku ya wanawake Dunia Machi 8 ambayo uazimishwa Kila mwaka wimbo huo utawauganisha wanawake pamoja .
"Haikuwa wepesi wasanii hawa wanawake kuungana lakini kutokana na mapenzi waliyonayo kwa Rais wa Samia wameamua kuonesha ustahimilivu wao na kuja pamoja na kutunga wimbo unaoamsha hali za wanawake kuungana na kushirikiana kwa pamoja"amesema









