-ya kuendeleza ujuzi waliopata chuoni na kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza wakati wakukabidhi vifaa hivyo Mratibu wa mradi wa Chaguo langu haki yangu, Joyce Kessy amesema changamoto kubwa ambayo bado wanahitaji kukabiliana nayo kielimu ni wazazi kushindwa kutoa ushirikiano ilikuhakikisha watoto wao waliopata mimba za utotoni wanapata elimu ya kujiendeleza kufikia malengo yao licha ya sasa kuwepo na mabadiliko makubwa toka kuanza kuchukua mabinti 84 waliohitimu na wengine 50 tayari wameshawasili vyuoni.
"Tumechukua na kuwapeleka mabinti 84 kusoma awamu ya kwanza na awamu ya pili tumechukua mabinti 50, hivi karibuni natunatarajia kuchukua mabinti 100 kupeleka veta na wote niwa Butiama na tunafanya hivi kwa lengo la kukabiliana na ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni na ukeketaji kwa mikoa ya Shinyanga na Mara" amesema Kessy.

Wakipokea msaada huo baadhi ya mabinti wamelishukuru shirika hilo la WiLDAF kwakuwasaidia kwani wengi wao walikuwa wakiishi maisha magumu kutokana na vitendo vya unyanyasaji na wengine wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na migogoro ya kifamilia na sasa wanatimiza ndoto zao kwa kusoma ufundi na kisha kukabidhiwa vifaa hivyo kwao wameona nifaraja kwani sasa watajitegemea.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mwalimu Mosse Kaegele amewataka wazazi kuachana na vitendo vya ukatili kwa watoto nakuwa sehemu ya kuwasaidia wanapopata changamoto huku akiwataka kutumia fursa waliyoipata kwa shirika hilo kufanya kazi kwa nidhamu na weredi mkubwa.










