Kaimu Mkurugenzi wa TPSF Raphael Maganga, amesema hayo leo Januari 5, 2024 Jijini Mwanza katika kikao kilichoandaliwa na Waziri wa Madini Antony Mavunde kililenga kukuza uwezo wa cha watoa huduma migodini.
Kwa upande wa Maganga alilisitiza kuwa uwepo wa sera unganishi ya taifa Ya ushirikishwaji wa Tanzania kama mwarobaini wa kuongeza ushiriki wa watanzania.
“Sera ya sasa ipo kwenye sekta za madini na Mafuta, sekta nyingine bado hazina sera ya Ushirikishwaji wa Tanzania (Local Content) hivyo, ili kuratibu ushiriki wa watanzania lazima kuwepo na Sera au sheria ya Taifa ya Ushirikishwaji wa Tanzania (National Local Content Policy). “
Aidha kwa upande wake Mavunde amesema zaidi ya kampuni 750 zinatoa huduma katika migodi mbali mbali Tanzania, Serikali kupitia Wizara ya Madini imedhamiria kuweka mikakati ya kuongeza ushiriki wa watanzania katika shughuli za madini ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya watanzania wanaotoa huduma na usambazaji wa bidhaa migodini.










