Hospitali ya Tumbi yaomba wadau kuwachangia damu

05Dec 2023
Julieth Mkireri
Pwani
Nipashe
Hospitali ya Tumbi yaomba wadau kuwachangia damu

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi, imewaomba wakazi wa mkoa huo kujitokeza Desemba 09, Mwaka huu ili kuchangia damu ambayo itasaidia kuokoa wagonjwa wanaofika kutibiwa katika Hospitali hiyo.

Tatu Gemela.

Kwasasa hospitali hiyo inatumia chupa 15 za damu kwa siku na 450 kwa mwezi na hivyo kuwa na mahitaji makubwa ya damu na kwasiku wanatokea wagonjwa 13 hadi 15

Mkuu wa kitengo cha damu salama wa Hospital hiyo, Tatu Gemela amewaomba wananchi na Taasisi za mkoa huo kujitokeza kwa wingi kuchangia damu siku hiyo.

"Wakazi wa ndani na nje ya mkoa tujitokeze tuokoe maisha ya wagonjwa na hapa tumezungukwa na makambi ya Jeshi tunaomba mtufikie tupate damu nyingi zikidhi uhitaji wanaofika kutibiwa katika hospitali yetu" alisisitiza.

Amesema uhitaji katika Hospitali hiyo ni mkubwa hasa kutokana na kuwa katika eneo la barabarani na kuhudumia wagonjwa wengi wakiwemo mama wajawazito na wanaopata ajali ambao ndio wanahitaji damu kwa wingi.