Katibu wa Chama cha riadha Mkoa wa Geita, Saguda Maduhu, ameiambia Nipashe Digital kuwa mbio hizo zimefana kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi waliojitokeza kushiriki kwenye tamasha la "Chato Utalii Festival" na kwamba zimezingatia sheria taratibu na kanuni za michezo huo.
Akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo, Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhandisi Deusdedith Katwale ameonyesha kufurahishwa na maandalizi ya mbio hizo huku akiahidi kuboresha mashindano hayo mwakani kwa kuongeza zawadi za washindi.
Mashindano ya Chato Utalii Festival yameandaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo yakiwa na dhima ya kukusanya fedha kwaajili ya kuondoa upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari wilayani humo.