Akizungumza katika hafla hiyo ambayo imetanguliwa na utiaji wa saini mkataba wa ujenzi wa daraja hilo kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) na Mkandarasi.
Mchengerwa amesema daraja hilo ambalo litajengwa kwa miezi.18 litagharimu sh.bilioni 11.5 na litawaondolea kero wnafunzi waliokuwa wanakwama kuhudhuria masomo wakati wa mvua.
Kadhalika Mchengerwa amesema ujenzi wa daraja hilo ni moja ya kitu ambacho kitainua uchumi wa wananchi wa maeneo hayo ambao wataweza kufika kila aneo kwa urahisi na kusafirisha bidhaa zao.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan mkoa huo umepokea sh. trilion 1.19 za miradi ya Maendeleo kati ya hizo sh.bilioni 102.1 ni za Miundombinu ya barabara kwa Wakala wa Barabara TANROADS na TARURA.
Ameeleza kwamba kati ya fedha za miundombinu fedha za Tarura ni sh. bilioni 49.3 na kwamba kitendo cha Serikali kutoa zaidi ya sh.bilioni 11 ujenzi wa daraja hilo unakwenda kufungua uchumi katika eneo hilo ambalo limekuwa kikwazo cha usafiri hususani kipindi cha mvua.
Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema daraja hilo hadi kukamilika litagharimu sh.bilioni 11.5 na kwamba litakuwa na urefu wa Mita 80 na kwamba litajengwa kwa miezi 18.
Pia amesema daraja hilo ambalo litajengwa kwa fedha za ndani likikamilika litadumu kwa miaka 100 litakuwa na makaravati mawili na barabara unganishi zenye urefu wa KM 1..










