Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dk. Jim Yonazi wakati akifungua mkutano wa wadau wa kilimo na lishe katika kuangalia maboresho ya program ya kuendeleza kilimo awamu ya pili (ASDP II) (2019/2028) wakati wa kukamilisha mpango kwa miaka mitano mwaka 2023.
Dk. Yonazi amesema dhana ya Serikali ni kuwekeza katika kilimo na kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwatoa wananchi kwenye umaskini katika sekta ya kilimo nchini.
Awali Mratibu wa Taifa wa (ASDP II) inayoratibiwa na ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Salim Nandonde alisema awamu ya kwanza walifanikiwa zaidi kwenye suala la ujenzi na maeneo ya miundombinu ya umwagiliaji na kuleta matokeo mazuri yaliyoyatarajiwa.
Alisema matokeo ya kikao hicho yatasaidia maboresho ya mipango ya miaka mitano ijayo ya program hiyo ya ASDP II.










