CHANETA yazindua ligi daraja la pili mpira wa pete

29Oct 2023
Neema Hussein
Nsimbo
Nipashe Jumapili
CHANETA yazindua ligi daraja la pili mpira wa pete

MASHINDANO ya mpira wa Pete Ligi Daraja la Pili kitaifa, yamezinduliwa katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi ambapo timu zaidi ya 10 kutoka mikoa mbalimbali zinatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Pete Tanzania (CHANETA), Dokta Devota Marwa amesema umuhimu wa mashindano hayo ni kuwapa fursa watoto wa kike kujiajiri kupitia mpira.

Amesema mashindano hayo hayataishia ndani ya nchi pekee yanatoa fursa za wachezaji kushiriki timu ya Taifa ambayo badae itawakilisha kimataifa.

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Anna Lupembe amesema haijawahi kutokea mpira huo kuchezwa Katavi ni mara ya kwanza kupokea timu 15 kutoka mikoa mbalimbali kuja kucheza Katavi

Amemuomba Mwenyekiti wa CHANETA kutembea nchi nzima kuhamasisha mpira wa pete, wilayani, shule za msingi na sekondari ili  mchezo huo uendelee kukua.