Katika taarifa iliyotolewa na timu hiyo, imeeleza kuwa, mchezaji huyo ataungana na timu yake baada ya makubaliano binafsi na dirisha la usajili kufunguliwa rasmi.
Ikumbuke siku chache zilizopita, Rais Samia Suluhu Hassan alitoa wito kwa Viongozi wa Yanga kulimaliza suala la Fei Toto, alipowaalika Ikulu kwenye hafla ya Chakula kuwapongeza kwa kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF).










