Hayo yalisemwa mapema wiki hii na na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Manyoni, Ahmed Makele, wakati wa kikao cha viongozi na wananchi wa wilaya ya Manyoni.
Kamanda Ahmed alitoa wito kwa serikali ya kijiji na ndugu wa marehemu kuendelea kutoa ushirikano ili kuhakikisha mchakato huo unaenda salama.
Alisema TRC imefanya jambo la msingi kwa kuanza kutoa elimu kwa wafiwa juu ya utaratibu utakao tumika kuhamisha makaburi hayo, akisisitiza kuwa hatua hiyo itaondoa migogoro kati ya serikali na wananchi.
“Nitoe wito kwa viongozi na wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika mchakato huu na hatimaye kazi iendelee” alisema.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo, Hassan Simba, alisema yeye na viongozi wenzake watatoa ushirikiano kwa TRC na mkandarasi wake kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.
“Reli hii ikikamilika itarahisisha shughuli za kijamii na kilimo kwa wakazi wa Manyoni pamoja na kuongeza kipato kwa kuwa watu watatumia usafiri huo kupeleka bidhaa sehemu mbalimbali,” alisema.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa dini walioshiriki mchakato huo, Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Itigi, Chiristopher Kiwango, aliishukuru TRC na uongozi wa wilaya kwa kuzingatia haki za binadamu, sheria na misingi ya imani wakati wa kuhamisha makaburi.
“Tunaishukru serikali kwa kutupa viongozi waliosimamia mchakato huu ambao umefanyika kwa utaratibu uliozingatia mambo ya afya, imani za marehemu pamoja na haki za binadamu, hivyo tunamshukuru Mungu lakini pia shukrani ziende kwa wale wote walioshiriki katika kazi ya kuhamisha makaburi,” alisema.










