Akizungumza katika kikao cha pili cha kuwasilisha rasimu ya mpango mkakati wa matumizi bora ya ardhi kilichofanyika eneo la Msaginya halmashauri ya Nsimbo Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Mipango Matumizi ya Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango Matumizi ya Ardhi Dioscory Kanuti amesema kikao hicho kimeshirikisha wadau mbalimbali lengo nikuchukua maoni yao na kuyafanyia kazi.
Kanuti amesema uandaaji wa mpango huo ulianza Julai 24 kwakuanza na rasimu ya mpango na Agosti 29 waliwasilisha rasimu hiyo kwa wadau kwaajili ya kupata maoni na kupendekeza dhana kati ya dhana tatu ambazo walizipendekeza.
"Dhana hizo ndio zitakua zinatoa uelekeo wa ukuaji wa halmashauri ya Nsimbo kwa kipindi cha miaka 20 ijayo,kwaiyo kama mlivyoshuhudia wadau walikua na hamasa kubwa ya kuchangia kulingana na rasimu ilivyowasilishwa na wametoa maoni na mapendekezo," amesema Kanuti.
Nae Afisa Mipango Miji na Vijiji kutoka halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Jude Shirima amesema mbali na mpango huo kuondoa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji au makazi na misitu pia kuna miradi mbalimbali ambayo imependekezwa kwenye mpango huo.
Shirima amesema endapo miradi iliyopendekezwa katika mpango huo wa halmashauri ikitekelezwa itachochea kasi ya uchumi katika halmashauri hiyo.
Amesema kwenye halmashauri ya Nsimbo kuna vijiji 54 na vijiji vinee ndio vimeandaliwa mpango bora wa matumizi ya ardhi ambavyo ni vijiji vitatu katika kata ya Ugala na kijiji komoja kilichopo kata ya Stalike.
"Vijiji hivyo ni kijiji cha Kasisi,Katambike Mnyamasi,na kijiji cha Igongwe vijiji hivi kuandaliwa matumizi bora ya ardhi vilifadhiliwa na wadau," amesema Shirima.
Amesema kutokana na ufinyu wa bajeti ya halmashauri wameshindwa kuandaa wenyewe mipango ya matumizi bora ya ardhi kutokana na gharama zinazohitajika hivyo amekaribisha wadau mbalimbali ambao wanaweza kufadhili mipango hiyo kwa vijiji ambavyo vimebaki.
Kwa upande wao baadhi ya wadau waliochangia katika kikao hicho wameomba mpango huo ukianza kutumika usimamiwe kuanzia gazi za kata, vijiji na vitongoji kupitia wenyeviti na watendaji.
Maiko Kasanga ni Diwani wa kata ya Nsimbo ni miongoni mwa wadau waliochangia ambapo amesema mpango huo wameupokea vizuri na watahakikisha wanawapa elimu wananchi wajue maana ya matumizi bora ya ardhi.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadan amesema wasipo usimamie mpango huo kila siku watalalamika eneo halitoshi.
Amesema eneo hilo likipangwa wananchi watalima,watafuga na wataishi endapo mpango huo ukisimamiwa ipasavyo.










