NIPASHE JUMAPILI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango (wa pili kulia) akikabidhi tuzo ya utambuzi kwa uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Theobald Sabi (wa pili kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo kufanikisha maendeleo ya sekta ya viwanda nchini katika tuzo za 16 za Rais kwa vinara wa Uzalishaji viwandani (PMAYA) zilizoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI).
Afisa wa Idara ya Huduma Mbadala Kupitia Mifumo ya Kidigitali wa Benki ya Exim Bw Gregory Malembeka (wa kwanza kushoto) sambamba na maofisa wengine kutoka Bodi ya taifa michezo ya kubahatisha nchini (GBT) wakizungumza na washindi wa droo ya kampeni “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja wake kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini.
Mshindi wa kwanza wa Bodaboda katika Kampeni ya Mastabata – Kotekote ya Benki ya NMB, Asumwisye Mwajeka (wapili Kushoto) akiijaribu pikipiki baada ya kukabidhiwa katika benki ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa.
Kushoto ni Meneja mwandamizi wa Idara ya Biashara za Kadi, Manfredy Kayala, kulia ni Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mkwawa, Happiness Pimma na wapili kulia ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu, Manyilizu Masanja.
