NIPASHE JUMAPILI
Mkuu wa Kitengo cha Bia wa Kampuni ya Serengeti (SBL), Nandy Mwiyombella akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa shindano la DJ compee, Take a Bite Out of Life, Mussa Shaban maarufu Dj. Son kutoka mkoa wa Kilimanjaro.Shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti Tanzania SBL lenye lengo la kuwasaidia vijana kuweza kujiajiri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa uongozi wake, Mkoa wa Mjini Magharibi jana. Kulia ni Makamu Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla na Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman (katikati). PICHA: IKULU
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kushoto) akishuhudia uwekaji saini ya makubaliano kati ya NMB na kampuni ya Bima ya Britam juu ya kutoa Bima kwa Wavuvi na Vyombo vyao maarufu kama Jahazi. Wanaotia Saini ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara Filbert Mponzi(wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam Raymond Komanga (tai nyekundu) katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Bima NMB - Martin Massawe
