Akizungumza baada ya mechi hiyo kumalizika, Mwambusi alisema walitawala kila kitu, wakati wakiwa wote 11 na hata baada ya kucheza pungufu, lakini umakini wa wachezaji wake uliwagharimu kwani mpaka mapumziko timu yake ilitakiwa iwe na mabao matatu.
"Nasikitika, tumepoteza mechi ambayo tulitakiwa kushinda, tulicheza dakika nyingi tukikiwa pungufu, nawapongeza tu Azam kwa bao walilolipata, lakini walikuwa kwenye mazingira magumu, tumetawala mechi, tumefanya mashambulizi, ila umakini unakosekama.
"Nafasi tatu za wazi tumepata, lakini umakini umekosemana, na hili itabidi tulifanyie kazi sana kwenye uwanja wa mazoezi, siyo kitu kizuri na tupo sehemu mbaya. Ligi ni ngumu na ina timu chache," alisema kocha Mwambusi.




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






