Hivi karibuni, vyombo vya habari Ulaya na Afrika vilifuatilia ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Suella Braverman nchini Rwanda, kufanikisha mipango ya kuhamisha wakimbizi au wahamiaji wasiotakiwa nchini Uingereza.
Serikali ya Rwanda katika kujiamini zaidi, ikalipokea hilo wahamiaji hao kutafutiwa makazi. Ni wakati Rwanda ilipojiunga na Jumuia ya Madola, ikiwa haiko tayari kuendelea na sura yake ya jadi ya 'kuwa mwanachama wa nchi wakoloni wa Ufaransa au Francophonie’.
Taifa hilo ni nchi yenye mwelekeo wa lugha ya mfungamano ya utamaduni na Ufaransa na mtawala wake katika ukoloni, kwani Ufaransa na Ubelgiji zina utamaduni sawia.
Utayari wa Rwanda kupokea wakimbizi hao una thamani katika maeneo mawili;kwanza kuwawezesha kuanza maisha mapya kwa walioona wamekwama
kwa sababu ndoto zao ni kujiunga na jamii za Ulaya, iwe Italia, Ugiriki, Uingereza, Ufaransa au Ubelgiji. Upinzani mkali ukatolewa kwao, hivyo mpango huo kwenda Rwanda ukaja ‘watake wasitake’ au warudishwe makwao.
Vikundi vya haki vya binadamu vimejitahidi kuweka pingamizi mahakamani nchini Uingereza vikakwama, sheria ikisema hilo lipo katika madaraka ya serikali, au katika uwezo wa nchi mbili kuliamua.
Eneo jingine, ni hitaji la nchi ndogo kuwa msaada kwa mataifa makubwa, yaani ushirikiano wa pande mbili zinazohitajiana, siyo tu wadau wa maendeleo au watoa misaada, kila wakati wakitokea Ulaya kuisaidia Afrika.
Rwanda imeamua kuonyesha mfano wa kuisaidia Uingereza katika mazingira, ambayo isingeweza kusaidiwa na nchi ya Ulaya. Upinzani wa kuwapo wakimbizi, wanabadili sura ya nchi na hali yake ya jadi. Ni suala gumu kisiasa kwa Ulaya na hata Marekani.
Wapinzani wa mpango huo ni wale ambao ukiwaambia Uingereza ni nchi ya Wazungu wanakuona mbaguzi, wakati kila nchi inajivunia utaifa, pale inapokaribisha wageni.
Jitihada za kuhamia kwingine zimepamba moto katika nchi nyingi ambazo hazina uwezo wa kihisia, kiimani, kinadharia au kisiasa wa kubadili mifumo yao ya jamii kuwezesha mabadiliko ya haraka na kuishi kama Ulaya.
Watawala na wasomi Afrika hawahangaishwi na sera gani zitawezesha hali kama hiyo kuwepo Afrika. Wanajitahidi kulinda Afrika ibaki na mali zake 'zisiporwe' na watu wa nje, halafu kila mmoja anajitahidi awatangulie, na hata awazodoe, ndugu zake kwa mali.
Licha ya matumizi ya kawaida ni vigumu kusema kuna kitu kama asasi za kiraia barani Afrika, ambako jamii inaona kero kwa wizi wa mali ya umma, uonevu na kujinufaisha, kunakozuia uwezo wa kufikiria mifumo au sera bora zaidi.
Waafrika na Waarabu wamefungwa katika dhamira zao kuhusu watakacho katika maisha ya jamii, hivyo maendeleo yanapatikana kwa kujikongoja, na balaa kubwa za kutoaminiana.
Ni katika mazingira hayo ambako baadhi ya vijana na hata wenye umri wa kati, mara kadhaa wanafanya kila wawezalo, hata kuuza amana ndogo walizo nazo katiambaadjio ya nchi, kupata fedha kuingia katika safari hatarishi za kuvuka Jangwa la Sahara na Bahari ya Mediterannean hadi fukwe za nchi za Ulaya.
Wakifika huko yapo makundi ya watetezi kwanza kuwaokoa baharini, kuwatafutia hifadhi halafu na msaada wa kisheria kujieleza ili wabakizwe Ulaya.
Taarifa za televisheni za Marekani zinasema takriban asilimia 90 ya waomba hifadhi nchini humo wanakataliwa. Hivyo wanaishia jela, wapewe fedha kidogo ya kujikimu, wapandishwe kwenye ndege kurudishwa makwao, au nchi waliyotumia kuingia.
Hoja ya msingi ya wapinzani wa mkakati wa Rwanda na Uingereza ni kuwa Uingereza inaikana hali ya ukimbizi au kuomba hifadhi, wakati kinachotokea hapa ni kuikimbia mifumo mibovu ilyojaa umaskini na mikwamo ya kisiasa inayoleta mafarakano au vita isiyoisha.
Wengi kati yao wamekuwa wakipinga 'kupendelewa' kwa wakimbizi kutoka Ukraine kuwa wanatofautishwa na wale wa Syria au Afghanistan.
Halafu nchi kama Marekani 'zikijiongeza' kuingia humo kurekebisha hali, dunia nzima haiko tayari kwa uvamizi kama huo. uliberali wa kimataifa unataka nchi ziamue jinsi zinavyojiendesha.
Labda ni kudhani kuwa nchi hizi ni mbumbumbu kwani demokrasia inawazuia kulinda ustahimilivu na utengamano wa aina ya jamii waliyo nayo, au labda umbumbumbu ni kudhania kuwa tukiharibu Afrika tutaenda Ulaya. Suala la msingi ni kama itafika siku Afrika ibadilike.
Kwa maana hiyo Rwanda kutoa mwanya wa mahali pa kuhamishia wakimbizi ni msaada muhimu kwa serikali ya Uingereza, kwani inajua Waingereza wakiendelea kujaziwa wakimbizi watachagua serikali za kifashisti kuwaondoa, na utengamano kijamii uwe mashakani.
Wapo wengi wasiopenda mifumo ya kibepari na utawala wa kidemokrasia Ulaya, wenye mipango ya mabadiliko makubwa kijamii na kudhania kuwa demokrasia itadumu hata baada ya hapo, na wengi tu hawajali hatari zinazotokana na kupokea mawimbi ya wakimbizi.
Rwanda inajua hawatafurika kwao, na watakaokuja wataingiza fedha za mfukoni kwao na za Uingereza kuwezesha uhamiaji huo. Ni ku-beti kimkakati wakiona kuna faida ya wazi.




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






