Mkataba na DP World siyo wakwanza nchini

15Jun 2023
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mkataba na DP World siyo wakwanza nchini

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa mkataba wa Tanzania na DP World sio mkataba wa kwanza nchini, mwaka 2000 serikali ya awamu ya tatu iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji na Kampuni ya Kimataifa ya Uendeshaji wa Vitengo vya Makasha, Hutchison ya Hong-Kong China.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.

Ambapo mkataba huo ulidumu kwa miaka 22 kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2022 na uliipa haki Kampuni hiyo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kuhudumia makasha katika gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam wakati maeneo mengine yakiendelea kuhudumiwa na TPA.

"Upangishaji huu uliendea kwa awamu zote na mwaka 2017, tulifanya mabadiliko makubwa kwenye mkataba wa mpangaji huo na December 2022, serikali ya Awamu ya Sita baada kuona mkataba huo hauendeni na matarajio ya serikali kuhusu maslahi mapana kwa nchi, iliamua kusitisha mkataba huo." ameeleza Mbarawa.

Top Stories