Amesema anaamini vijana wakipata mafunzo yatawaandaa kushika uongozi katika sekta mbalimbali za mataifa yao na yatawasaidia kuongeza uelewa na kuleta matokeo chanya.
Kinana aliyasema hayo jana wakati akifunga programu ya mafunzo kwa viongozi vijana, kutoka vyama sita vya wapigania uhuru nchi za kusini mwa Afrika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani.
“Kazi ya kuwalea vijana ni pamoja na kuwafunza, kuwasamehe pale wanapokosea , kuwasahihisha ili wapate taaluma ya uongozi na kuwa viongozi bora wa kuongoza wananchi wa nchi zetu.
“Tuache kutumia lugha kuwa vijana ni taifa la kesho, vijana sio taifa la kesho, vijana ni viongozi wa leo lazima tuwape nafasi ya kuongoza,” alisema
Alisema asilimia 70 ya Watanzania na nchi nyingi Afrika ni vijana na ni viongozi wa sasa, hivyo ni vyema waaminiwe na kupatiwa nafasi ya kuongoza.
Kinana pia alikishukuru Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa kuendelea kushirikiana na vyama hivyo. Alisema CCM itaendelea kudumisha umoja na ushirikiano baina ya vyama tawala vyote.
Vyama vilivyoshiriki katika katika mafunzo hayo CCM kutoka Tanzania, SWAPO (Namibia), MPLA (Angola), ZANU - PF (Zimbabwe) , ANC (Afrika Kusini) na FRELIMO cha Msumbiji.




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






