Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Meneja wa chapa wa konyagi fusion, Pamela Kikuli alisema: “Tunayofuraha kutangaza kuwa leo tunazindua kinywaji kipya cha konyagi. Kama mnavyojua konyagi imekuwa na historia kubwa tangu ilipoanzishwa miaka ya 1968, kwa sasa tumeleta konyagi zenye ladha mbili tofauti kwa ajili ya vijana wa kisasa”.
Alisema Hatua hiyo ni mwendelezo wa chapa ya konyagi fusion kwamba lengo na dhumuni la Tanzania Distilleries Ltd ni kuwafanikisha wateja wao wanapata ladha tofauti na waliyoizoe.
Alisema konyagi fusion ina asilimia 20 ya kilevi na inapatikana katika ujazo wa milimita 250.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, Timea Chogo alisema wakati wanafanya uchunguzi waligundua kwamba mojawapo ya mitindo ya kimataifa ya vinywaji vya pombe ni kutumia ladha mbalimbali katika pombe kali.
Alisema: “Hivyo tukaamua kutumia kinywaji chetu cha kizalendo kutengeneza kinywaji kipya kinachofuata mitindo ya kimataifa. Konyagi fusion zinatumia ladha za kusisimua na pia kuburudisha. Tuna Imani kubwa wateja wetu watazipenda ladha hizi mpya’.
Alisema kinyaji hicho kitazinduliwa Februari 17, mwaka huu katika ukumbi wa Tipsy Coco jijini Dar es Salaam, kwamba wateja watapata fursa ya kuburudika kwa sababu ni mara ya kwanza kuuzwa kwa chupa za milimita 250.




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






