Msemaji wa klabu hiyo Jerry Muro alisema kuwa, kocha huyo amechangia kwa kiasi kikubwa kwa wao Yanga kutopambana na Simba kwenye mechi ya fainali ya kombe hilo lililochezwa mjini Zanzibar kuanzia Januari 2 hadi 13.
"Ningeshangaa kama asingefukuzwa.
Yeye kwa kiasi kikubwa amechangia sana kutokuwepo kwa mechi ya Simba na Yanga mwaka huu. Tulitegemea tutakutana fainali, lakini kitendo cha Simba kufungwa na Mtibwa bao 1-0 kwenye mechi na nusu fainali kilifanya wachezaji wa Yanga kushuka morali kwenye mechi ya baadaye dhidi ya URA," alisema Muro.
Alisema kama Simba ingeingia fainali, anadhani kuwa hata wachezaji wa Yanga wangecheza kwa nguvu na bidii kubwa kuweza kushinda ili kukutana na watani wao wa jadi.
"Tena kwenye mechi dhidi ya Mtibwa ndiyo haikucheza vizuri kabisa, nadhani Kerr alikuwa na hofu ya kukutana na Yanga, akaona heri nusu shari kuliko shari kamili," alisema na kuongeza.
"Kwa kiwango kile ningeshangaa kusikia bado yupo," alisema Muro.
Hata hivyo, alisema iwapo Yanga ingekutana na Simba kwenye mechi ya fainali kwa kiwango walichonacho sasa, walikuwa na uhakika wa kurudisha magoli 5-0 waliofungwa mwaka 2012.
Wakati Simba ikitolewa na Mtibwa kwa bao 1-0 Jumapili jioni, majira ya usiku Yanga iliondolewa kwa mikwaju 4-3 na URA baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Simba imemtimua Kerr kwa kile ilichodai ni kushindwa kuifanya timu hiyo iwe na matokeo ya kuridhisha kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na Ligi Kuu, pamoja na kiwango duni inachokionyesha tangu kuichukua timu kutoka mikononi mwa Goran Kopunovic.
Tungeshangaa Kerr asingetimuliwa-Yanga
17Jan 2016
Taifa Letu
Tungeshangaa Kerr asingetimuliwa-Yanga
KLABU ya Yanga imesema ingeshangaa iwapo watani wao wa jadi wasingemtimua kocha wao mkuu Dylan Kerr kutokana na kiwango cha chini walichokionyesha kwenye Kombe la Mapinduzi.
Aliyekuwa Kocha wa Simba, Dylan Kerr (wa pili kushoto)




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






