Wakizungumza baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, wamesema kuwa inasikitisha kuona klabu kubwa kama Simba yenye hadhi kubwa barani Afrika, ikiwa na kikosi duni, kinachocheza kana kwamba ni klabu ya madaraja ya chini.
Mwanachama wa siku nyingi wa klabu hiyo Majaliwa Mbasa alisema kuwa anachokiona ni kwamba viongozi wameshindwa kazi yao ya uongozi, hivyo kwa sasa hawana cha kufanya ila ni kusubiri miaka yao iliyobaki ya uongozi imalizike ili wachague wengine.
"Ukweli ni kwamba wameshindwa kazi. Kikosi kinaonekana kabisa hakipo sawa. Simba ni mbovu kuanzia kipa hadi nafasi ya ushambuliaji. Haieleweki inacheza mfumo gani, kusema kweli inasikitisha sana," alisema Mbasa.
Alisema kuwa hata kama kocha mkuu Kerr akituhumiwa kuwa ndiyo chanzo, lakini kocha huyo kama hana uwezo, lakini ameletwa na viongozi hao hao ambao amedai kuwa hawapo makini.
"Tukilaumu wachezaji inabidi tujiulize, wamesajiliwa na nani? Na kama ni kocha, naye ameletwa na kina nani?," alihoji mwanachama huyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Simba tawi la Mpira Pesa Ustaadhi Masoud yeye lawama zake moja kwa moja alizipeleka kwa kocha Kerr na kumshangaa kwa kukosa kikosi kwa kwanza hadi leo hii.
"Kocha inaonekana hana kikosi cha kwanza hadi sasa, wachezaji ambao wanaonekana kuwa wangeibeba timu anawaweka nje, leo anapanga hawa, kesho hawa, kusema kweli hatumuelewi," alisema.
Simba imekuwa si tu kwamba haifanyi vizuri kwenye mechi zake kwa sasa, lakini pia hata kiwango kimekuwa hakiwaridhishi wanachama na mashabiki wa timu hiyo.
Simba Luwala yakera wanachama wake
17Jan 2016
Taifa Letu
Simba Luwala yakera wanachama wake
KIWANGO kisichoridhisha kulichoonyeshwa na kikosi cha Simba kwenye michuano la Kombe la Mapinduzi kimewakera wanachama na mashabiki wa klabu huyo, kila mmoja akizungumza lake lakini lawama zaidi zikielekezwa kwa viongozi na kocha mkuu Dylan Kerr ambaye tayari ametimuliwa.
Mashakini wa Simba




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






