Hali hiyo imejitokeza baada ya gazeti hili kutaka kufahamu kiasi gani cha fedha hadi sasa kimepelekwa katika akaunti za shule kwa ajili ya elimu bure kama alivyoahidi Rais Dk.John Magufuli ambapo katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk.Silvacius Likwelile
alisema wizara yake imetoa kiasi hicho kwa ajili ya kugharimia chakula, ada, ruzuku na gharama za mitihani ya kidato cha nne.
Bila kusema wizara yake imeelekeza fedha hizo katika wizara gani kati ya wizara hizo, alisema serikali kupitia wizara ya fedha na mipango imejipanga kuhakikisha kuwa ahadi ya Rais Magufuli inatekelezwa bila kusuasua.
“Wajibu wa wizara yangu ni kuidhinisha fedha, ufafanuzi juu ya matumizi ni jukumu la wizara zinazohusika na elimu wasiliana nao,” alisema Likwelile.
Hali ilikuwa tofauti baada ya kumtafuta Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kuhusu kiasi gani cha pesa kimeshatumwa shuleni kabla ya kufunguliwa kwa shule,
alisema fedha hizo zinaratibiwa na Tamisemi na kwamba wizara yake haihusiki.
“Unajua wizara yangu haihusiki kabisa kuratibu pesa za ruzuku wasiliana na Tamisemi watakupatia majibu na kama fedha hizo ni sehemu ya bajeti ya wizara yangu kwa mwaka 2015/2016,” alisema kwa ufupi.
Kisha gazeti hili likamtafuta katibu Mkuu wa Tamisemi, Jumanne Sagini lakini katika hali ya kushangaza naye akatupa mpira kuwa kuhusu uratibu wa fedha hizo kwa kusema kuwa mratibu wake ni wizara ya elimu ingawa awali Prof. Ndalichako alisema haihusiki.
“Tafadhali mpigie simu Naibu katibu Mkuu wa Elimu kwa ajili ya kutoa ufafanuzi mimi sina jibu kwa sasa,” alijibu kwa mkato.
Gazeti hili halijabaini chanzo cha wizara hizo kutupiana mpira kuhusu kuratibu fedha hizo za ahadi ya Rais ingawa hofu ya kuchukuliwa hatua kwa matumizi mabaya ya fedha hizo kama rais Magufuli alivyowaonya wakuu wa shule watakaotumia fedha hizo kwa mambo mengine mwanzoni mwa Desemba mwaka jana.
Hata hivyo alipokutana na waandishi wa habari mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka jana Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene alisema fedha hizo zitaratibiwa na wizara yake na kutaja kiasi cha fedha kuwa kimetengwa na serikali kwa ajili ya kutekeleza ahadi ya raia ya elimu bure.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Simbachawene alisema kuwa pamoja na serikali kutangaza elimu bure lakini mzazi atakuwa na jukumu la kununua sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu na nauli.
Nyingine ni gharama za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa na kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi kwa wanafunzi wa bweni.
Baadhi ya shule zilizotembelewa na gazeti hili jijini Dar es Salaam ili kujua maendeleo ya utekelezwaji wa ahadi hiyo, baadhi ya walimu kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini walidai kuwa wana taarifa za uhakika kuwa fedha hizo hazijatumwa kwenye akaunti za baadhi ya shule huku wengine wakisema wameanza kupokea mgawo wa awali.
Mawaziri wa Magufuli wazikwepa bil.18 elimu bure
17Jan 2016
Leonce Zimbandu
Taifa Letu
Mawaziri wa Magufuli wazikwepa bil.18 elimu bure
IKIWA imebaki juma moja kabla ya kufunguliwa shule za msingi na sekondari hapa nchini kimeibuka kitendawili kuhusu nani msimamizi wa kiasi cha Shilingi bilioni 18.777 za ruzuku ya elimu bure baada ya wizara mbili, Elimu,Teknolojia na Ufundi na Ofisi ya waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutupiana mpira.
Waziri wa Elimu,Teknolojia na Ufundi Pro. Joyce Ndalichako




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






