Wakati hayo yanatokea, wagombea wa nafasi hiyo wamekimbilia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kutaka kujua hatma ya uchaguzi huo.Machi 6, ilikuwa siku ya kufanya uchaguzi jijini Dar es Salaam ambapo wajumbe wote 142 wa mkutano mkuu, walikuwa wametua lakini wakiwa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Magomeni Usalama, ghafla wakaambiwa zoezi limeahirishwa.Tangazo la kuahirishwa kwa uchaguzi, lilitolewa na Katibu Mkuu, Richard Lyimo na kusababisha sintofahamu huku wajumbe wakihoji imekuwaje uchaguzi uahirishwe ghafla bila kuwapo maelezo ya kutosha.Baada ya uchaguzi kuahirishwa katika mazingira hayo, wagombea wa nafasi hiyo, Aivan Maganza na wenzake Kananzaro Mwanga, Stanley Ndamugoba na Abuu Changawa, waliandika barua kwa Msajili.Sehemu ya barua hiyo inasomeka; "Sisi wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa taifa wa TLP, tunaleta malalamiko yetu kwako kuhusu kuvunjwa kwa mkutano mkuu maalaum wa uchaguzi, kujaza nafasi ya mwenyekiti wa taifa wa chama, ambao ulikuwa ufanyike Jumatatu ya tarehe 6, Machi 2023, kwenye ukumbi wa Legho Hotel, kwa visingizio visivyo na ukweli wowote."Maganza ambaye anawakilisha wagombea wenzake anasema barua ya kuvunja mkutano wa uchaguzi ilikuwa imesainiwa na Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho.Anafafanua katika barua hiyo kuwa bodi haina mamlaka ya kupinga maamuzi ya Halmashauri Kuu ya chama iliyokutana Mei 5 mwaka huu na kupitisha ya wagombea na kuamua uchaguzi ufanyike Machi 6 mwaka huu, ambapo ni kwa mujibu wa Katiba ya TLP ibara ya 18:5h(i) na kutaka maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa yaheshimiwe.Barua hiyo inamalizia kwa kuelezea; "Hivyo tunakuomba Msajili wa Vyama vya Siasa uamuru uongozi wa TLP uitishe mkutano mkuu maalum haraka iwezekanavyo, ili demokrasia ndani ya chama itekelezwe."HOJA ZA MSAJILIMsajili wa Vyama vya Siasa, baada ya kupokea malalamiko hayo, anaulima barua uongozi wa TLP a kiutaka ujieleze ni kwa nini uliahirisha uchaguzi wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho.Barua hiyo ya Machi 9, mwaka huu yenye Kumbukumbu HA. 322/362A/38, ambayo imesainiwa na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, inaelekezwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Richard Lyimo, kuwasilisha maelezo katika ofisi hiyo.Nyahoza anaeleza katika barua hiyo kuwa Ofisi ya Msajili, imepokea barua kutoka kwa baadhi ya wagombea wakilalamikia kuahirishwa kwa mkutano mkuu bila kufuata katiba na kanuni za chama hicho.Aidha, barua hiyo inaendelea kueleza: "Kwa mujibu wa kifungu 5B cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, uongozi wa TLP mnapaswa kuwasilisha maelezo kwa Msajili kujibu malalamiko ya wagombea hao." Barua hiyo inaeleza kuwa majibu ya uongozi wa TLP yatasaidia kumfanya Msajili wa Vyama vay Siasa kujua ukweli kuhusu sakata hilo.Wakati barua ikielezea hayo, mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti Taifa, Mhandisi Aivan Maganza, anasema yeye na wenzake watatu waliaamua kuchukua hatua hizo ili kuhakikisha haki inatendeka.
Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi hiyo, akithibitisha kupokea barua hiyo na kufafanua kuwa ataijibu kama alivyoelekezwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
WANACHAMA WAFOKAMmoja wa wajumbe kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Esta Mlay, analalamikia kitendo hicho na kudai kimeleta usumbufu na kutaka uongozi kuendelea na uchaguzi akisema ni aibu kwa chama chao kukaa muda mrefu bila mwenyekiti.Katibu wa TLP Mkoa wa Dodoma, Damari Richard alisema kuahirishwa kwa uchaguzi huo kunatia shaka, kwa kuwa siku moja kabla walimaliza mkutano wao wa ndani kwa amani, lakini akashangaa kuona uchaguzi unaahirishwa."Hiki ni chama kikubwa, na sisi ni wajumbe kutoka miaka mbalimbali, tupo kwenye chama hiki kwa miaka mingi, lakini mambo kama haya yanatia aibu na tunapoteza imani kwa wafuasi wetu," anasema Damari.
VIASHIRIA VYA RUSHWAWakati lawama zikielekezwa kwake, Katibu Mkuu Lyimo anadai kuwa kuahirishwa kwa uchaguzi huo kulitokana na kuwapo kwa viashiria vya rushwa kwa viongozi wanaowania nafasi hiyo.Kulikuwa na shida kwa baadhi ya viongozi kwenye chama chetu, kwani tulishuhudia Naibu Katibu Mkuu, anatukanwa matusi ya nguoni na mmoja wa wagombea akimwambia yeye ni 'mwizi, mpumbavu na anakula rushwa mbele ya viongozi wa (TLP) Moshi, iliniuma sana," anasema Lyimo.Lyimo ambaye pia ni mgombea wa nafasi hiyo, anasema baada ya kuahirisha uchaguzi huo, watakaa vikao vya ndani kupanga muda, kwa kuwa ni lazima wawe na mwenyekiti."Wanachama, wapenzi pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu, wajue kuwa haya ni mambo ya kisiasa yaliyo nje na uongozi, tunaahidi kuitisha tena uchaguzi kwa sababu wagombea watakuwa walewale,"anasema.Chama hicho kiko katika mchakato wa kufanya uchaguzi huo ili kujaza nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mwenyekiti wa TLP Taifa, Augustine Mrema, ambaye alifariki dunia Agosti mwaka jana.Nafasi hiyo kwa sasa inakaimiwa na Hamad Mkadam aliyechaguliwa na sekretarieti ya chama hicho Septemba mwaka jana, ikiwa ni wiki chache baada ya Mwenyekiti Mrema kufariki dunia.




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






