...maarufu kama Bilionea Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyella, maarufu kama Ray hadi Februari 23, mwaka huu saa 3:00 asubuhi.
Mjane huyo kwa mara ya kwanza alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Oktoba 23, 2016 akidaiwa kumuua wifi yake, Aneth Msuya, aliyeuawa Mei 26, 2016 kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam.
Aneth alikuwa mdogo wa Bilionea Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni, Hai mkoani Kilimanjaro, Agosti 7, 2013.
Katika utetezi wake, Mrita alidai kuwa hawezi kumuua Aneth kwa sababu alikuwa kama mtoto wake wa kuzaa na kwamba alipoolewa yeye (Mrita) na mume wake walikabidhiwa wamlee tangu akiwa shule ya msingi
Hukumu hiyo ilipangwa kutolewa jana na Jaji Edwin Kakolaki baada ya mahakama kumaliza kusikiliza ushahidi wa mashahidi 25 wa upande wa mashitaka, utetezi, vielelezo na kupitia vifungu vya sheria.
Desemba 11, 2023 wakati wazee wa baraza (Iddi Humba na Omary Panzi) wanatoa maoni yao, waliishauri mahakama iwaachie huru washtakiwa kwa sababu hawana hatia.
Mzee Humba alidai kuwa amepitia ushahidi wa mashahidi 25 na ushahidi wa upande wa utetezi katika mashahidi watano wa utetezi na kujiridhisha kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka bila kuacha shaka yoyote.
Mzee Panzi kwa upande wake, alidai kuwa baada ya kusikiliza pande zote anaunga mkono maoni ya mwenzake kuwa amejiridhisha kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka bila shaka yoyote.
Jaji Kakolaki baada ya kusoma muhtasari wa ushahidi wa kila shahidi wa pande zote, alisema katika jinai kuna mambo makuu mawili ya kuangalia kitendo chenyewe ambacho mshtakiwa anakuwa anatuhumiwa kukitenda ni kwamba lazima kithibitike.
Pia alisema ni kusudio la mtu kutenda kitendo au kosa hilo na kwamba hayo mambo yote mawili ndiyo yanatengeneza kosa.
Katika maelezo ya onyo ya Miriam anadaiwa kueleza kuwa aliamua kumuua wifi yake kwa sababu alikuwa anamfuatafuata katika suala la usimamizi wa mirathi ya mumewe, marehemu Bilionea Msuya, na kwamba katika kutekeleza mauaji hayo, alimkodi mtu ambaye alimlipa Sh. milioni 20.
Maelezo hayo ya Miriam yalisomwa mahakamani hapo na shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, Sajenti Mwajuma, aliyemhoji mshtakiwa huyo na kuandika maelezo yake alipotiwa mbaroni, baada ya kupokelewa mahakamani hapo kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.
Hata hivyo, Miriam katika utetezi wake alikataa maelezo hayo na kudai kuwa kwanza hawezi kumuua wifi yake Aneth kwa sababu alikuwa mtoto wake wa kumlea tangu akiwa shule ya msingi hadi anaolewa na pia hakuwahi kuwa na ugomvi wa mali au mirathi na wifi yake huyo.
Shahidi wa 25 wa upande wa mashitaka, Getruda Mfuru, ambaye alikuwa dada wa kazi wa Aneth, alidai kuwa Mrita alimwahidi kumpa Sh. bilioni 50 kama angekamilisha kazi ambayo anaitaka kuifanya na dada yake.




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






