Mtu kama atashindwa kuwa msafi katika biashara ambayo anafanya, anaweza kuwaambukiza wateja wake maradhi yatokanayo na uchafu. Mnapokimbiwa kutokana na uchafu huo, hakuna wa kumlalamikia.
Ikitokea mtu anajihisi mambo yake hayaendi vizuri katika kazi zake, kikubwa anachokitanguliza mara zote ni malalamiko ‘kuna mkono wa mtu.’
Kabla hujafika huko kwenye dai la ‘mkono wa mtu,’ Je, umeishafanya utafiti kwa nini wenzako wanafanikiwa na wewe hufanikiwi? Ukifanya utafiti utaona tatizo ni wewe na sio ‘mkono wa mtu.’
Mambo hayo yapo ya ‘mkono wa mtu,’ lakini kuna wakati mwingine sio mkono wa mtu, bali wajihi na mwonekano wako, ndio utakaofanya watu wasipende kutumika bidhaa zako kutokana na uchafu wako.
Hivi abiria gani atakataa kupanda chombo cha mtu aliye msafi na akapanda cha kwako wewe usiyependa usafi?
Ikitokea abiria kapanda kwako sio kwamba anakushabikia sana, bali amekosa usafiri na ana haraka. Hivyo, katika hali ya kawaida akifika ‘kijiweni’ kwenu, ni lazima atawafuata wasafi na kukuacha wewe ambaye ni mchafu, maana mwonekano wake unaudhi wateja.
Nianze sasa kuwarudisha katika mada ambayo nataka kuizungumzia katika hili la bodaboda ambao usafiri wao unatumiwa na watu wengi, kwa ajili ya kuwawahisha waendako.
Baadhi ya madereva wa bodaboda wameshindwa kabisa kujiweka katika hali ya usafi, wakati wanajua wazi wanabeba wateja kwa kuwapeleka ofisini na hata katika kufuatilia mahitaji na mambo mbalimbali.
Yaani unakuta dereva wa bodaboda kavaa kandambili, kakata kiduku au ‘dreds’ eti yupo kituoni kusubiria abiria. Nani atakufuata kukukodi?
Sasa uvaaji huo utamfanya abiria ambaye yeye kavaa vizuri utakuwa na imani ya kubebwa na wewe?
Mwonekana wa mtu mchafu unamtisha abiria, hata hawezi kivutiwa nawe. Anaona ni bora amchukue mtu ambaye yupo katika mwonekano nzuri.
Najua katika changamoto pale mvua zinaponyesha, mteja huwa hachagui chombo, atakuchukua tu, lakini msingi mkuu kwamba hana chaguo.
Mteja hawezi kukubali kubebwa na mtu ambaye hayupo katika mwonekano nzuri. Najua, huenda au yawezekana wapo wakaopinga haya ninayosema.
Lakini naelewa katika ukweli ulikosimama, kwamba hali hiyo inaweza kuwa kweli katika kipindi cha mvua, lakini kama sio mvua, hawezi kupata mteja.
Kuna vijana wanaopenda kuvaa kama nyie. Wao watapenda muwabebe, lakini kumbukeni kuwa vijana hao sio waendaji kazini na hata dau lao linakuwa sio kubwa.
Ushauri wangu kwenu madereva wa bodaboda ni kwamba mjipende, jambo ambalo naamini la gharama kubwa.
Kwa nini msinzingatie usafi? Mbona madereva wa teksi wapo katika mwonekana mzuri, kwa mini nyie msiwaige hao wenzenu wazoefu katika fani?
Madereva wa teksi pamoja na kuwa ndani ya gari, huwezi kumuona kanyoa ‘kiduku’ au kasuka nywele katika hali isiyovutia na kushinda na ndala.
Hiyo inawafanya wapendwe na watu, hata kuwakodi na kuwapeleka katika maeneo mbalimbali.
Nyie ndugu waendesha bodaboda, yaani mtu ambaye chombo chake kipo wazi, anaona na kila mtu eti kavaa kandambili, kaptula, kasuka ‘dreds’anavaa na fulana chafu, halafu anatafuta wateja.
Kuna haja ya kujitathmini nyie weaendesha bodaboda, kwani hiyo ni ofisi inayokuingizia kipato na kukufanya ubadilishe mlo wewe au wewe na familia yako. Lazima ukajitunza.
Mwisho.
Top of Form
Bottom of Form