Methali hii hutumiwa kumshauri mtu mwenye nia ya kuongeza maarifa yake kwamba asione ugumu wa kujifanya mnyonge ili afaidike.
Ufafanuzi huu ni maalum kwa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kuruhusu vilabu vya Ligi Kuu kusajili wachezaji wengi kutoka nchi za nje. Kwani Tanzania haina wachezaji wenye uwezo kama au kuliko wao? Wapo wengi ila tunashindwa namna ya kuwapata na kuwafunza itakiwavyo.
Tunaambiwa “chako ni chako, cha mwenzio si chako.” Kitu unachokiita chako ni kizuri na huweza kukufaa na una uhuru nacho kuliko cha mtu mwingine. Twafunzwa kuvitegemea vitu vyetu wala sio vya watu wengine.
TFF yapaswa kuanzisha chuo maalum cha mafunzo ya kandanda kwa vijana wanaopenda mchezo huo. Chuo hicho kiwe na walimu wazawa watakaoongozwa na wataalamu wa kandanda na daktari wa viungo kutoka nje ya nchi. Kwa utaratibu huo Tanzania yaweza kupata wachezaji mahiri wa kandanda watakaoisaidia nchi na hata kutakiwa na vilabu vya Ulaya.
Nashindwa kuelewa ni kwa nini TFF imeruhusu vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kusajili wachezaji wa kigeni hadi kumi kwa msimu mmoja.
Nashindwa kuelewa ni kwa nini TFF imeruhusu vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kusajili wachezaji wa kigeni hadi 10 kwa msimu mmoja! Kwa nini isiwe wachezaji wawili au watatu ili kuwapa nafasi wachezaji wetu? Baadhi ya wachezaji wa kigeni hawana tofauti na wachezaji wetu na mara nyingine wachezaji wetu huonekana kuwa bora zaidi ya wageni.
Kupunguza wingi wa wachezaji kutoka nje utawanufaisha wachezaji wetu kwani watapata nafasi ya kucheza nje ya nchi kwa kusajiliwa na vilabu vikubwa vya Uingereza, Ujerumani, Italia, Hispania, Ufaransa n.k. Hii itakuwa manufaa kwa pande zote mbili yaani Tanzania na wachezaji watakaosajiliwa nnje ya nchi.
Tusihadaike na rangi, tamu ya chai ni sukari. Maana yake tusidanganyike kutokana na rangi ya chai kwani utamu wake hutokana na sukari. Methali hii yaweza kutumiwa kumkanya mtu kutopumbazwa au kutovutwa na sifa za nje za kitu ila akichunguze kwa ndani.
Wachezaji wageni wanaocheza kandanda nchini, hasa timu za Azam, Simba na Yanga ni wangapi huitwa makwao kuzichezea timu za mataifa yao? Labda ni wawili tu waliosajiliwa na Simba kutoka Uganda na mmoja kutoka Rwanda ndio huitwa kuzitumikia timu zao za taifa zinaposhiriki michezo ya kimataifa.
Waliobaki huja Tanzania kujitafutia maisha baada ya kushindwa kuzivutia timu za Ulaya na Afrika. Wengine, kama twakumbuka, walijileta wenyewe nchini kutafuta timu za kuwasajili. Iliposhindikana walirejea kwao kimya kimya na njaa zao!
Tanzania imegeuzwa kuwa ‘jalala’ la kupokea ‘makapi’ kutoka nnje nasi kuwapapatikia kama afanyavyo kuku anayechinjwa! Kama wangekuwa wa maana wangesajiliwa na vilabu vikubwa vya Afrika na Ulaya kama walivyo kina Mbwana Samatta na wengineo.
Msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara umemalizika kwa Simba Sports Club wanaofahamika pia kama ‘Wekundu wa Msimbazi,’ kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo. Cha kushangaza ni kuwa imetwaa ubingwa huo ikiwa kwenye mji wa Singida kama ilivyokuwa msimu uliopita!
Tofauti ni jinsi ilivyokuwa msimu uliopita na huu uliomalizika majuzi. Msimu wa mwaka jana, Simba iliutwaa ubingwa wakati wachezaji wake wakiwa hotelini kutokana na Yanga kufungwa 1-0 jijini Mbeya na Tanzania Prisons.
Msimu uliomalizika hivi karibuni, pia Simba ilitwaa ubingwa ikiwa Singida pia kwa kuifunga timu hiyo mabao 2-0 ingawa bao la pili lilikuwa na mushkeli (kasoro). Hata kama lisingekubaliwa, bado Simba ni bingwa kwa bao la awali lililofungwa na mshambuliaji wao hatari, Meddie Kagere mapema kipindi cha kwanza na kukosa majibu ya wenyeji, Singida United.
“Mambo yafaayo watu ni yaingiayo chunguni.” Maana yake mambo yanayofaidi watu ni yanayoingia chunguni. Hutumiwa kumtanabahisha mtu kuwa njia nzuri ya kumsaidia mtu aliye shidani ni kumkabidhi kitu sio kumpa ahadi au kumtolea maneno matupu tu.
Viongozi wanapaswa kufahamu kuwa “Ahadi ni deni (na deni ijuzie).” Maana yake ahadi ni kama deni, mtu akitoa ahadi lazima aitimize. Methali hii yatufunza umuhimu wa kutimiza ahadi tutoazo. Wachezaji wasifanywe kama watoto wadogo wasiojua maana. Viongozi wawe makini kwa ahadi watoazo.
“Dama ni iliyo mkononi.” Dama ni aina ya kamba inayotumiwa kufungia tanga la chombo cha baharini. Maana yake dama inayoweza kutumiwa au kumfaa mtu ni aliyo nayo mkononi. Kitu kinachoweza kumfaa mtu ni alichonacho karibu wala sio kilicho mbali.
0784 334 096