TOTO YAUA

24Jan 2016
Lete Raha
TOTO YAUA

Timu ya Toto African ya Mwanza jana iliibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Pamba ya Mwanza kwenye mchezo wa kusisimua wa Kombe la Shirikisho linaloendelea hivi sasa kwenye viwanja mbalimbali.

Toto Africans ya Mwanza

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Toto ilitawala vyema dakika za mwanzoni za kipindi cha kwanza na kupata mabao mawili kupitia kwa washambuliaji wao Miraji Athumani (dakika ya 7) na Waziri Shentembo (dakika ya 26). Pamba walicharuka na kupata bao katika dakika ya 45 kupitia kwa James Sungura.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wachezaji wa Toto na Pamba wakishambuliana kwa kupokezana na ndipo dakika ya 56, Miraji Athumani aliandika bao la tatu kwa upande wa Toto kabla ya straika Edward Christopher kumalizia bao la nne alilolifunga dakika ya 79.

Top Stories