Guu la kulia ni hatari mabao ligi kuu Bara

29Aug 2023
Adam Fungamwango
Dar es Salaam
Nipashe
Guu la kulia ni hatari mabao ligi kuu Bara
  • Chama, Onana na Baleke waubeba mguu wa kushoto huku ya kichwa yakiwa...

IK I W A mechi 13 za Ligi Kuu Bara zimeshapigwa hadi sasa, jumla y a mabao 29 yamezamishwa nyavuni huku yaliyofungwa kwa mguu wa kulia yakiwa mengi zaidi kuliko yaliyotokana na mguu wa kushoto na kichwa.

Chama.

Mabao hayo 23 yamefungwa ndani ya boksi na sita yamefungwa nje ya eneo la hatari huku mawili yakiwa ni kwa faulo na moja la kona. Kwa mujibu wa Kitengo cha Takwimu Michezoni cha Nipashe, mabao 18 yamefungwa kwa mguu wa kulia na saba yakifungwa kwa mguu wa kushoto wakati matatu yakiwa ya vichwa na moja la kujifunga mwenyewe kwa kipa wa Coastal Union, Justin Ndikumana kwenye mechi kati ya timu yake dhidi ya Dodoma Jiji FC ambayo walilala 2-1.Mabao ya faulo kwenye Ligi Kuu mpaka sasa yamefungwa na Ibrahim Ajibu kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, zikitoka sare ya bao 1-1, Agosti 20, Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro, lingine likifungwa na Martin Kigi wa JKT Tanzania katika mechi iliyochezwa Agosti 15 dhidi ya Namungo, Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi na likiwa bao pekee, maafande wakishinda 1-0. Maguri wa Geita Gold ndiye mchezaji pekee kwenye Ligi Kuu aliyefunga bao lililotokana na mpira wa kona. Ilikuwa katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo msimu huu dhidi ya Ihefu alipopachika bao pekee, akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliyopigwa na Edmund John. Mabao sita katika mechi hizo 13 yaliyofungwa nje ya kisanduku cha hatari, Ajibu akiwa mchezaji pekee aliyefunga bao kwa umbali mrefu zaidi akifanya hivyo kiasi cha takriban mita 35 katika mechi ambayo timu yake ya Coastal Union ilicheza dhidi ya Mtibwa Sugar, huku mengine yakizamishwa na Kigi wa JKT Tanzania, Meshack Abraham wa Dodoma Jiji, Adam Adam na Othman Dunia wote wa Mashujaa na Mudathir Yahaya wa Yanga. Wakati wachezaji 16 wakiongozwa na Feisal Salum wa Azam FC na Mathew Antony wa Mtibwa Sugar kila mmoja wakifunga mawili, wakipachika 18 kwa mguu wa kulia kwenye ligi mpaka sasa, jumla ya wachezaji saba wamefunga mabao saba kwa kutumia mguu wa kushoto. Wachezaji hao ni Clatous Chama, Willy Onana na Jean Baleke wote wa Simba, Adam Adam na Othman Dunia wa Mashujaa FC, Hija Ugando wa Coastal Union na Rashid Chambo wa KMC.

Top Stories