Wamebainisha hayo leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari ambao walifika kuona daraja hilo, na kueleza adha ambayo wanaipata baada ya daraja hilo kukatika.
Mmoja wa wananchi hao Joseph Machiya, amesema kutokana na daraja hilo kukatika wamekuwa wakipata tabu kupita kwenda mjini kufuata mahitaji, huku wanafunzi wakihatarisha maisha kwa kupita katika maeneo ambayo ni hatarisha kwa kusombwa na maji.
“Tunaiomba Serikali itufanyie matengezo ya haraka ya daraja hili ili lipitike na hata kunusuru maisha ya watoto wetu wakati wa kwenda shule,”amesema Joseph.
Mwananchi mwingine Gudeha Chambalo, amesema kwa sasa wamekuwa wakipata shida kwenda mjini kwenye mahitaji mbalimbali, na wamekuwa wakipita kwenye daraja hivyo hivyo ambalo limekatika.
Nao baadhi ya Madereva wa Bodaboda akiwamo Joseph Mahona, wamesema wamekuwa wakipata shida kupita kwenye daraja hilo, huku wananchi wengine wakipita juu ya Reli Hali ambayo ni hatari endapo wakifumanizwa na Treni.
Naye Meneja Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani Shinyanga Mhandisi Samson Pamphil, amesema miundombinu mingi ya barabara pamoja na madaraja imeharibiwa na mvua, na kubainisha kwamba kwa sasa wanasubili bajeti ipite pamoja na mvua kupungua ili waanze kufanya matengenezo ya miundombinu ambayo imeharibiwa na mvua.




.jpeg?itok=vCj6bCRe)






