Dudu hazitaki mbichi hizi?

01Jun 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Dudu hazitaki mbichi hizi?

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Godfrey Tumaini 'Dudubaya', amewataka wasanii wenzake ambao wamekuwa wakienda nje ya nchi kuandaa kazi zao watoe pesa hizo ili kuwasaidia wenye shida.

Godfrey Tumaini 'Dudubaya'

Amesema inashangaza kuona wasanii wanakubali kutumia gharama kubwa kwenda kufanya kazi nje na kuwaacha wataalam wa hapa nchini, ambao ni wazuri na huenda kuzidi hao wa nje.

"Wanachokifanya wasanii hao ni sawa na kuwadharau watayarishaji wa muziki wa hapa nchini, kama wanaona wana pesa nyingi ni bora wakawapa wahitaji," alisema Dudubaya.

Alisema kuwa kwake yeye haitatokea siku moja kufanya hivyo na kwamba ataendelea kuwatumia watayarishaji wa hapa hapa nchini na ndiyo waliotengeneza wimbo wake mpya wa 'Kokoriko' ambao umeanza kufanya vizuri.

Top Stories